Kabla ya kuanzishwa kwa THTU, Chuo Kikuu cha Dodoma, kulikuwa na chama kimoja tu cha wafanyakazi RAAWU, ambacho hata hivyo kilikuwa na wanachama wachache sana na sehemu kubwa ikiwa ni wafanyakazi waendeshaji. Wanataaluma wakiwa hawafiki hata watano, na timu nzima ya Uongozi ikiwa imejaa administrators. In short ilikuwa imeelemea upande mmoja zaidi. Lakini pia viongozi wake walishindwa kabisa kusaidia wafanyakazi kutatua matatizo yao kwa wakati, hali hii ilijidhihirisha pale ambapo UDOMASA, ililazimika kufanya kazi kama Trade Union, ambayo kimsingi haikustahili.
Ilipoanzishwa THTU, mwezi February wanachama zaidi ya 100 walijiunga. Kikiwa na uwiano mkubwa sana wa wafanyakazi wandeshaji. Hata safu ya uongozi, nusu wakiwa wanataaluma na nusu wafanyakazi waendeshaji. Mwezi wa Marchi tuliomba rasmi tawi kufunguliwa, na tukakubaliwa tukiwa na wanachama zaidi ya 150, wanachama ambao RAAWU, ilikuwa haijafikia na mpaka leo hii bado haijafikia.
Mnamo mwezi May, tuliomba THTU, itambuliwe kama Mwakilishi wa wafanyakazi, tulijaza form kwa ajili ya Exclusive Bargaining Right, na tukakabidhi utawala. Kwa mujibu wa sheria za kazi ilitakiwa tuwe tumejibiwa ndani ya siku 30. VC alitushauri tuondoe suala la muda. Tufanye majadiliano, kwa sababu chuo kwanza ni kichanga, pili ni mara ya kwanza taasisi inakuwa na chama zaidi ya kimoja, Ushauri ambao tuliupokea bila shaka yoyote, nia yetu ikiwa ni kujenga.
Suala hili tangu hapo, limekuwa likipigwa danadana, na hata sasa limechukua miezi minne, bila mafanikio. Mnamo 19 August 2011, tulifanya mkutano na ofisi ya STC, kwa ajili ya kuhesabu wanachama RAAWU walikwa na wanachama 139 tu, wakijumuisha na wanachama ambao walishajitoa, na THTU ilikuwa na wanachama 255. Cha kushangaza baada ya mwezi , yaani 19 Septemba, tukaitwa tena, tukahesabu wanachama kwa ajili majina yamejirudia. Tukatumia busara tukaenda kikao ambacho Mwenyekiti wa RAAWU, hakutokea, akamtuma Katibu wake nae hakutokea. Na hata walipopatikana wajumbe wawili wa kamati yao ya utendaji na mwanachama mmoja, walikataa kufanya mkutano huo. Tukiwa na Mwenyekiti wa UDOMASA, tukaliripoti hili kwa VC, ambae ameamuru suala hili liishe Alhamisi 22, Septemba 2011, ameagiza Ofisi ya DVC PFA, HR, STC, RAAWU, UDOMASA tukutane. Tumekwisha pokea barua kwa ajili ya mkutano huo.
Cha kuchekesha wanachama RAAWU, iliyowaweka amabo si wao ni wengi, Lakini yupo mwanaharakati na mpiganaji mzoefu, ambae pia ni Katibu wa THTU, Bwana Fredrick Oywech, yupo Balozi Lipili, yupo Mwanamama mpambanaji Kuluthum Mchatta, hao ni baadhi tu. Barua zao za kujitoa RAAWU, niliziwasilisha mimi mwenyewe.
Lazima niweke kumbukumbu sahihi, pamoja na juhudi za wazi za Makamu Mkuu wa chuo kutaka suala hili liishe, kumekuwa na njama za makusudi kabisa, ambazo nitazieleza vizuri kabisa wakati wa kutoa comment. Sisi kama THTU, tunaandaa ripoti yetu juu ya hili suala , na msimamo wetu, kwa Mujibu wa sheria za kazi. Naomba niwahakikishie hili suala litafika mwisho. Tumeazimia baada ya mkutano huo, tusiporidhika tutalipeleka suala hili CMA (Court of Mediation & Arbitration), siku ya Ijumaa asubuhi. Hili tutalisimamia kwa uwezo wetu wote. Hadi sasa THTU ina wanachama zaidi ya 300, wafanyakazi waendeshaji wakiwa zaidi ya 100,ambayo ni zaidi ya asilimia 33 (33%), mchakato unafanyika majina yao yataonekana humu muda si mrefu. Wenzetu kwenye idadi yao hiyo ya 139, wanataaluma wapo 7 tu, ambayo ni asilimia 5 (5% tu)hii ni hatari sana kwa masilahi ya chuo, tusishangae pale UDOMASA inapobidi iwe Trade Union.
Nini msimamo wa THTU, juu ya hili suala? Siku ya Alhamisi jioni 22 septemba 2011, tuta-post kwenye hii blog yetu. Don’t Go away
Cheers MWERANGI, Iddy (Chairman)
THTU stands for The Tanzania Higher Learning Institutions Trade Union. It is an organisation registered on the 12th December 2008 (Reg. No. 23) under the Tanzania Trade Union Registration Act. THTU was established primarily to provide a national forum for Higher Learning Institutions' workers to deliberate on matters that affect workers welfare, Institutional welfare, productivity and broader community interests that impinge on their ability to participate effectivelly in national development.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tulifanya kikao na STC na wajumbe wa RAAWU,23 / Septemba / 2011 na tumekubaliana THTU ina wanachama wengi, hivyo tumekubaliwa kujaza form kwa ajili ya Exclusive Bargaining Right.
ReplyDeleteNimeshaijaza form, na kesho tutaikabidhi rasmi kwenye uongozi wa chuo, na tutakuwa tumepata majibu ndani ya siku 30, kama sheria inavyosema. Tunawaomba wafanyakazi wa UDOM, waendelee kutu-support ili tuweze kufikia malengo yetu.
NIA NA MWELEKEO WETU DAIMA NI KUJENGA
Fomu Na 2, kwa ajili ya kuomba kutambuliwa kama wakala pekee wa majadiliano tumeshaikabidhi, ofisi ya DVC-PFA,tangu 28th Septemba 2011 na taratibu zote za kisheria zimezingatiwa.
ReplyDeleteNIA NA MWELEKEO WETU DAIMA NI KUJENGA
Suala la Exclusive Bargaining Right, limeshakamilika! Na sasa THTU ndiye mwakilishi wa wafanyakazi.
ReplyDeleteTumewaagiza viongozi wetu wafuatilie yafuatayo:
1. Wahakikishe tunaanza kuwakilisha wanachama kwenye vikao
2. Baraza la wafanyakazi linavunjwa, na linaundwa lingine kwa mujibu wa taratibu za THTU.
3. Tawi lazima lihakikishe wafanyakazi kunakuwa na mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi. watu walipwe, Xtra duty, over time. na masuala ya nyumba iwe ni kwa wafanyakazi wote. hili linawezekana, mkiendelea kutuunga mkono
4. Chama lazima, kiingie makubaliano ya Pamoja na chuo kwa maandishi. Taratibu za nidhamu lazima ziwe wazi. Na wafanyakazi wasifukuzwe kiholela
Tayari chama kimeiandikia management kuomba kufanya nao mkutano kujadili pamoja na mambo mengine masuala hayo hapo juu!!!
NIA NA MWELEKEO WETU DAIMA NI KUJENGA!