Saturday, May 5, 2012

THTU WAKALA MAALUMU WA MAJADILIANO UDOM KUANZIA 3/ MAY 2012

Chama cha wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu (THTU), tawi la UDOM , kimepewa hadhi ya kuwa wakala pekee wa majadiliano kupitia barua ya Makamu Mkuu wa Chuo, Prof Idris S. Kikula yenye Kumb. Na. UDOM/VC/THTU/175/38. Hatua hii imefuatiwa baada ya kuwazidi wanachama chama cha RAAWU. Ambao uwakala wao ulisimama rasmi tarehe 3/May 2012. Sasa kila tunaposheherekea Sikukuu ya wafanyakazi duniani, tunajiandaa kusheherekea ushindi huu. Kwa niaba ya Kamati ya utendaji ya THTU, wanawashukuru sana wanachama wake kwa kuendelea kuwaunga mkono. Moto wetu kwa sasa ni kuhakikisha wafanyakazi wote waliofukuzwa wanarudi. Ajenda nyingine tutaanza kujadili kwa kina baada ya kufanya ukombozi wa wafanyakazi ambao wamefukuzwa kinyume na sheria. Chama kimejiandaa vyema. Na kinapenda kiwahakikishie hakuna mtu atakayepotea. Kwa taarifa zaidi tembela FACEBOOK PAGE

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.