Wednesday, September 14, 2011

NAMNA YA KUWASILISHA MALALAMIKO

Dear Members,

Kumekuwa na malalamiko kwa wanachama wetu, either wamepunjwa mshahara au kuna stahiki zao wamenyimwa. Lakini wengi wao wakiwafuata viongozi wa kamati ya utendaji kulalamika wakitaka msaada wa kufuatilia ili haki itendeke.

Napenda kuchukua fursa hii kutoa rai, namna nzuri ya kuwasilisha malalamiko yako, andika barua kwenda kwa

KATIBU WA TAWI,
THTU UDOM BRANCH.
P.O.BOX 1472,
DODOMA.

kwenye barua yako eleza vizuri hoja juu ya malalamiko yako, weka viambatanisho vyote muhimu, na ikabidhi mapema kwa Katibu, ambaye atatoa muongozo namna nzuri ya kushughulikia tatizo lako. Matatizo yatakayowasilishwa kwa mdomo tu, hayatashughulikiwa kwa kuwa hayana grounds kwa ajili ya ufuatiliaji. Ikiwa utakabidhi malalamiko yako kwa maandishi.

Tumeshazungumza na Katibu ndani ya siku 7, atakuwa ameshatoa muongozo juu ya kero husika.

NIA NA MWELEKEO WETU DAIMA NI KUJENGA

1 comment:

  1. Mbali ya anuani tajwa hapo juu, unaweza pia kutumia barua pepe ( thtu.udom@gmail.com ) au mpigie Katibu wa tawi kwa msaada zaidi ( +255759018000 )

    Tushirikiane na kuendelea kupeana mawazo, wanachama wapya form watazipata kwa wajumbe wote wa kamati ya utendaji.

    NIA NA MWELEKEO WETU DAIMA NI KUJENGA!

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.